Mahitaji: Ulinzi dhidi ya magonjwa ya mhogo.

 

Virusi vya magonjwa ya mimea vinaweza kuharibu hadi asilimia 100 ya mazao ya mihogo; kutishia maisha ya watu na kusababisha njaa. Aina za mhogo ambayo ina upinzani wa magonjwa yote zinaweza kuboresha mara moja uwezo wa zao hili wa kulisha na kuleta mapato kwa wakulima wadogo wa Afrika.

Uzalishaji wa mhogo Afrika umepunguzwa na magonjwa mawili ya virusi vya mimea:
Ugonjwa wa milia ya kikahawia (CBSD) ambao unaharibu mizizi inayoliwa hata wakati ambao sehemu nyingine za mmea zinaonekana zina afya nzuri, na ugonjwa wa mhogo wa kiasilia (CMD) ambao unaweza kudumaza mimea kwa kiwango tofauti au kuiua kabisa. Magonjwa haya mawili aghalabu hupatikana pamoja katika shamba moja na yanaweza kuharibu mazao yote. Magonjwa yote mawili huenezwa na nzi weupe (Idadi yao ikiwa kubwa sana ambayo haiwezi kudhibitiwa kwa kikamilifu na dawa za wadudu) na kwa mashina ya mihogo yaliyokatwa na wakulima kugawana kati yao.

CMD Leaf Symptoms

Mottled, misshapen & twisted leaflets with an overall reduction in size of leaves

CMD Root Symptoms

Severe decrease in root weight resulting in lower yields

CBSD Leaf Symptoms

Severe chlorosis & necrosis on leaves, giving them a yellowish, mottled look

CBSD Root Damage

Severe yellow/brown necrosis with a cork like appearance

 

 

Ugonjwa wa CMD umekuwa ukiharibu mashamba ya wakulima barani Afrika kwa miongo mingi. Zaidi ya miaka 15 iliyopita ugonjwa wa milia ya kikahawia (CBSD) nayo pia imeenea kwa kasi na sasa inaathiri uzalishaji wa mhogo katika Afrika Mashariki na Kati. Inatishia kuingia hadi Afrika Magharibi ambako itakuwa na madhara mabaya kwa uzalishaji wa mhogo na usalama wa chakula huko Nigeria, nchi ya kiafrika yenye idadi kubwa watu zaidi na mzalishaji mkubwa wa mhogo. Matokeo yake, ugonjwa wa milia ya kikahawia umetajwa kuwa mojawapo ya magonjwa saba ya mimea hatari, zaidi duniani kwa sababu ya athari zake zinazoendelea kuathiri chakula na usalama wa kiuchumi.

 

Uzalishaji wa mimea kwa njia za kidesturi umetumiwa kwa ufanisi kuendeleza aina za mihogo ambayo inapingana na ‘CMD’. Lakini wakuzaji wa mimea wamekuwa na mafanikio duni ya ugonjwa wa milia ya kikahawia- CBSD, na hivyo wameweza kukuza aina tu ambazo zinastahimili ugonjwa huo. Mimea ya mhogo inayostahimili CBSD ingali bado inaonyesha baadhi ya dalili za virusi na kupata uharibifu wa ugonjwa huu- huweza kusababisha ueneaji wa ugonjwa zaidi.

 

Kazi yetu: Kukuza aina za mihogo ambayo itakuwa sugu kwa magonjwa yote pamoja. Ugonjwa wa milia ya kikahawia (CBSD) na ugonjwa asilia wa mhogo (CMD)

 

Watafiti wetu wanatumia uhandisi wa maumbile kwa kutia sehemu ndogo ya virusi vya milia ya kahawia ya mhogo kwenye mimea ili kuifanya istahimili ugonjwa kwa mbinu inayoitwa kuingiliwa kwa RNA, (RNAi). RNAi imekuwa ikitumika kuendeleza idadi ya mazao sugu kwa magonjwa, hasa kuokoa sekta ya mapapai huko Hawaii kutokana na magonjwa makubwa ya virusi ya Ringspot.

Tumefanikiwa kukuza mhogo wenye nguvu kubwa na imara kustahimili ugonjwa wa milia ya kahawia “CBCD” kwa kutumia mbinu ya ugeuzi wa kijeni na kufanya majaribio kadhaa shambani huko Uganda na Kenya, kwa kibali, uangalizi na uongozi wa wasimamizi wa serikali.

Aina za mihogo ambazo zinastahimili ugonjwa asilia wa mhogo “CMD” tayari zimeanzishwa kwa kutumia uzalishaji wa mimea kwa hivyo mradi wa ‘VIRCA PLUS’ unafanya kazi ya ziada ya kuzalisha kwa kuchanganya zile aina zinazostahimili ugonjwa wa kiasilia ‘CMD’ pamoja na jeni za upinzani za mmea mwingine za milia ya kikahawia (CBS) zinazostahimili. Uendelezaji wa majaribio na upimaji wa aina hizi mpya unaendelea nchini Kenya.

Kenya na Uganda huhakikisha kwamba zinadhibiti magonjwa ya mimea na wakati huo huo zinazalisha mazao mazuri na kudumisha uteuzi wa wakulima kutegemea ladha, ulaini, usindikaji na uhifadhi.

Wakati sifa bainishi zinazohimili magonjwa ya virusi vya mhogo pamoja na aina za kuchanganya za ‘VIRCA PLUS’ na kuchunguzwa kikamilifu kwa usalama, wakulima watakuwa na uwezo wa kukuza mihogo yenye ukinzani maalum wa magonjwa yote kwa mara ya kwanza. Kenya, Uganda na nchi nyingine za Arika Mashariki zinatarajiwa kuwa na masoko ya awali ya aina zinazostahimili magonjwa za ‘VIRCA PLUS’.