Soma habari za hivi karibuni za maswala zinazohusiana na mradi wa uchunguzi wa VIRCA Plus

Jifunze matokeo yetu kama ilivyoripotiwa katika magazeti ya kisayansi

Jifunze zaidi kuhusu kazi yetu kupitia majibu ya maswali haya

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu mradi huu

Je, VIRCA PLUS ni mradi gani?

VIRCA PLUS ni mradi wa utafiti wa kuendeleza upinzani wa magonjwa ya virusi na aina za mihogo yenye lishe imara ambao utawawezesha wakulima wadogowadogo wa Afrika kuboresha hali ya afya ya watumiaji.

Mradi huu ulizinduliwa mwaka 2016. ‘VIRCA PLUS’ umeundwa kutokana na ufanisi wa miradi miwili ya awali. Mradi wa upinzani wa virusi vya mihogo katika Afrika ambao umefanikiwa kuendeleza upinzani mkali na imara dhidi ya ugonjwa wa mihogo wa milia ya kikahawia, uliohalalishwa baada ya mimea kuzalishwa kwa mzunguko ili kupata mazao mengi kwenye maeneo kadhaa nchini Kenya na Uganda.

Mradi wa ‘BioCassava plus’ uliendeleza na kupima mimea ya mhogo yenye chuma na zinki mara 10 zaidi ikilinganishwa na aina zingine, viwango vinavyoleta manufaa muhimu kwa watumiaji.
‘VIRCA PLUS’ inachanganya na kujumuisha ujuzi, uzoefu na matokeo ya miradi hii miwili ya awali ni kazi inayoendelea ya kuboresha mavuno ya mihogo na kutoa lishe bora huko Afrika Mashariki na Magharibi.

Kwa nini mihogo?

Mihogo hupandwa katika nchi zaidi ya 30 za Afrika. Takribani theluthi moja ya idadi ya watu barani Afrika hutegemea wanga wa mizizi ya mihogo kwa asilimia zaidi ya 50 ya matumizi yao ya kila siku ya kaloris (nguvu zipatikanazo ndani ya chakula) na kuufanya zao kuu la pili la chakula (baada ya mahindi). Pia ni zao muhimu la biashara ya wakulima wadogo kwa sababu linastawi vizuri katika hali ya joto na kwenye udongo usio na rutuba nyingi. Pia mhogo una manufaa ya kutengeneza nishatihai (biofuel), vinywaji na kusindika bidhaa pote Afrika zinazoleta masoko ya kutosha na mapato kwa wakulima.

Je, kuna tofauti gani kati ya mihogo ya VIRCA PLUS na aina nyingine za mihogo? Kwa nini mimea mingine inaonekana tofauti na jaribio ya mashamba?

Mihogo ya VIRCA PLUS ingefanana na aina zingine za mihogo ambazo wakulima wa mihogo wa Kenya , Nigeria na Uganda wamekuwa wakipanda tofauti tu ni kwamba ina uwezo mkubwa zaidi wa kupingana dhidi ya magonjwa na/au ina ubora zaidi wa lishe.

Watafiti wanatumia majaribio ya shamba ili kuendeleza aina bora zaidi kwa sababu mimea katika majaribio ya mashamba imezalishwa kutokana na mchanganyiko tofauti wa mimea ya wazazi inaonekana tofauti na nyingine. Wazalishaji huzalisha mimea mingi katika misimu mingi wakichunguza urefu, ukubwa wa mizizi na sifa nyingine ili waweze kuchagua ile ambayo itakidhi mahitaji ya wakulima.

Ni lini wakulima watapata mihogo aina za VIRCA PLUS?

Ni vigumu kukadiria muda maalumu wa kuendeleza aina za mihogo uamuzi wa kudhibiti hadi kumfikia mkulima. Mihogo inamzunguko mrefu wa ukuaji hii ina maana kwamba unachukua muda mrefu kuzalisha aina mpya. Ni lazima upitie kipindi cha miaka kadhaa ya ukuzaji ili kubaini, kuijaribu na kuiongeza aina zinazokidhi mahitaji ya wakulima. Zaidi ya hayo, wakati utakaochukua ili kukamilisha urejeshi wa udhibiti na uamuzi unaweza kuwa muda mrefu usio na hakika.

Kwa aina zinazopingana na magonjwa, majaribio ya shambani yanaendelea huko Uganda na Kenya ili kuchagua aina zilizoboreshwa na kuna matumaini kwamba mamlaka ya udhibiti itashughulikia usalama na ufanisi. Lengo letu ni kuwasilisha hali za udhibiti zilizo na maelezo yanayohitajika kuhusu upinzani wa virusi vya magonjwa ya mihogo ‘VIRCA Plus’ kuzifikisha kwa mamlaka ya udhibiti ya nchi hizo mbili katika 2019. Mapiti yao na idhini ni muhimu ili kuruhusu kilimo na vifaa vya kuzuia ugonjwa wa mihogo wa milia ya kikahawia. ‘CBSD’ kutumiwa na wakulima na wazalishaji kuitumia kama wazazi katika mipango ya kuboresha mazao ili kupata aina mpya zinazopinga CBSD- ugonjwa wa mhogo wa milia ya kikahawia.

Aina za lishe zilizoimarika zinatarajiwa kuanza kutathminiwa katika majaribio Nigeria 2018, na kufuata ukuzaji sawa na huo wa miaka mingi ya kupima na kufanya marekebisho.

Ni nani atakayedai umiliki wa mihogo ya ‘VIRCA PLUS’? Je wakulima watalipia? Wataweza kurudia kupanda tena?

Kama aina nyingine za mazao zilizokuzwa na mashirika ya kitaifa ya utafiti wa kilimo, mihogo ya ‘VIRCA PLUS’ itaweza kupatikana kwa bei nafuu kwa wakulima. Hakutakuwa na malipo au kizuizi cha haki kutoka kwa waendelezaji wa teknolojia yoyote: Kituo cha Sayansi cha Danforth au washiriki wa Shirika la Taifa ya Utafiti wa Kilimo nchini Kenya, Nigeria na Uganda. Mihogo ya ‘VIRCA PLUS’ itaachiliwa kwa wazilishaji mbegu kukuza zaidi aina mpya. Mihogo ya VIRCA PLUS inapotolewa kwa wakulima inaweza kupandwa, kukuzwa, kuliwa, kuuzwa na kupandwa tena kutoka kwa vipandikizi, kama ilivyo kwa sasa na kwa aina za kawaida.

Je mihogo ya VIRCA PLUS ina thamani ya kiuchumi sawa na mihogo mingine?

Kwa kuunganisha upinzani wa magonjwa mawili makubwa, inatarajiwa kwamba mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itakuwa na ufanisi mkubwa na thamani zaidi kiuchumi kwa wakulima kuliko aina za sasa ambazo zinaweza kuwa zimepungua ubora na hutoa mavuno machache kutokana na magonjwa.

Mihogo ya ‘VIRCA Plus’ iliyoimarishwa lishe inaweza kuwa na thamani kubwa zaidi kiuchumi kwa wakulima na watumiaji kutokana na faida za kiafya kwa sababu ya kuwa na madini ya chuma na zinki zaidi.

Ni nani aliyehusika na mradi wa VIRCA Plus? Wana wajibu gani?

Nchini Kenya, Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo nchini (KALRO) ndilo shirika linaloongoza shughuli zote za kiufundi na kimajaribio shambani.

Shirika la ISAA AfriCenter nchini Kenya linasaidia kuwafikia wadau. Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Kitropiki (IITA) nchini Kenya inafanya utafiti na shughuli za maendeleo.

Katika Nigeria, Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Mazao ya mizizi (NRCRI) huko Umudike hufanya utafiti na shughuli za maendeleo kuimarisha lishe ya mihogo ‘VIRCA Plus’. Shirika la Kitaifa la Maendeleo ya Bayotekinolojia (NABDA) linasaidia mawasiliano na kueneza shughuli zake nchini humo.

Katika Uganda, Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa mazao ya Kilimo (NaCRRI) ya shirika la Taifa la Utafiti wa Kilimo (NARO) ni shirika linaloongoza shughuli zote za kiufundi na za shamba. Ufadhili wa Sayansi ya Maisha na Maendeleo (SCIFODE) unaongoza mawasiliano na wadau kwa niaba ya mradi huo.

Kituo cha sayansi cha Donald Danforth huko St Louis; Missouri, Marekani huratibu mradi wa ‘VIRCA Plus’ kwa ujumla na pia hufanya shughuli za kimsingi za utafiti na maendeleo.

Ni nani anayechangia mradi wa ‘VIRCA Plus’?

Wafuasi wa sasa na wa zamani wa mradi wa VIRCA Plus ni pamoja na serikali za Kenya, Nigeria na Uganda, ufadhili wa Bill na Melinda Gates, ufadhili wa Howard Buffett, Bayer (ikiwa ni pamoja na kupitia kwa Mosanto na fedha za Monsanto ambazo zilipatikana 2018) na shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa. Ufadhili unatolewa kwa njia ya kugawana gharama na kutoa msaada ambayo haina faida za kifedha kwa wafuasi.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu upinzani wa magonjwa

Ni magonjwa gani ya mihogo unayoshughulikia na kwa nini ni muhimu

‘VIRCA Plus’ huendeleza mihogo ambayo ina upinzani wa magonjwa mawili ya virusi mara moja: Ugonjwa wa milia ya kikahawia (CBSD), ambao unaharibu sehemu ya mzizi inayoliwa wakati sehemu nyingine ya mmea inaonekana ina afya, na magonjwa asilia ya (CMD) ambayo yaweza kudumaza mimea kwa viwango vinavyotofautiana au kuiua kabisa. Magonjwa haya mawili hupatikana pamoja katika shamba moja na yanaweza kuharibu mazao yote. Magonjwa yote yanaenezwa na nzi weupe. (Idadi kubwa ya inzi haiwezi kudhibitiwa vyema kwa dawa za wadudu za kupuliza) na kwa njia ya mashina ya mihogo (vipandikizi) ambayo wakulima hugawana kati yao.

Ugonjwa asilia (CMD) umekuwa ukiharibu mashamba ya wakulima katika Afrika kwa miongo mingi. Kwa miaka 15 iliyopita, ugonjwa wa milia ya kikahawia umekuwa ukienea kwa kasi mno na sasa umeathiri mavuno ya mihogo katika Afrika Mashariki na Kati. Inatishia kuenea hadi Afrika Magharibi ambako itakuwa na athari mbaya kwa mavuno ya mihogo na usalama wa chakula nchini Nigeria, nchi ya Kiafrika yenye idadi kubwa na inayozalisha mihogo kwa wingi. Matokeo yake, ugonjwa wa milia ya kikahawia (CBSD) umetajwa kuwa kati ya magonjwa saba hatari zaidi kwa mimea duniani kutokana na athari zake zinazoendelea kwa chakula na usalama wa uchumi.

Je, mihogo inayopingana na ugonjwa wa virusi wa ‘VIRCA Plus’ utatoa kinga kwa magonjwa yote?

La. Hapana. Mihogo inayopingana na ugonjwa ya ‘VIRCA Plus’ imekusudiwa kulinda mazao dhidi ya magonjwa ya virusi- CBSD na CMD. Wakulima watahimizwa kuendelea na mazoea mengine mazuri ya usimamizi wa kilimo ili kutoa ulinzi dhidi ya magonjwa mengine ya ndani, wadudu, magugu na mambo mengine ya kimazingira ambayo yanaathiri uzalishaji.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu uimarishaji wa Lishe

Je, mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itakuwa na uimarishaji gani wa lishe?

Mradi wa ‘VIRCA Plus’ unaendeleza mihogo ambayo ina kiwango cha juu cha chuma na zinki kwa ajili ya kuboresha lishe, pamoja na kupambana na magonjwa na virusi vya magonjwa. Mradi wa mihogohai (BioCassava) (2005-2016) ulifaulu kuendeleza na kupima mimea ya mihogo ambayo ilikuwa na kiasi cha madini ya chuma na zinki kwa mara 10 ikilinganishwa na aina zingine, kwa kutumia zana za kisasa za bayotekinolojia. Wakati inapotumiwa kwenye mapishi ya vyakula vya kiafrika (kama vile gari na fufu), mihogo yenye virutubisho inaweza kutoa asilimia 40-70 ya kiwango cha wastani kinachohitajika cha madini ya chuma na zinki kwa wanawake na watoto wenye mazingira magumu (wanaoweza kudhurika).

Upungufu wa madini ya chuma huathiri mfumo wa kinga, unadumaza ukuaji na kuharibu utambuzi wa kiakili katika maendeleo ya watoto, wakati upungufu wa madini ya zinki unasababisha ongezeko la hatari ya vifo kutokana na kuharisha kudumaa na kuviza ukuaji wa utambuzi. Nchini Nigeria peke yake asilimia 75 ya watoto wa shule za mapema na asilimia 67 ya wanawake wajawazito wana upungufu wa damu (anemia) (kutokana Shirika la Afya Duniani 2008) na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inakadiriwa kuwa asilimia 24 ya Idadi ya watu wako katika hatari kutokana na upungufu wa zinki uliosababishwa na kutokula chakula cha kutosha (Prasad 2012).

Chanzo cha msingi wa madini ya chuma na zinki kwa watu maskini wa vijijini na mijini unapatikana kwa kula vyakula vya mimea hasa aina za maharage, mboga za majani, na nafaka nzima (isiyokobolewa). Hata hivyo, upatikanaji wa kiasi kinachohitajika cha vyakula hivi mara nyingi ni vya kimsimu na hakuna uhakika wa ubora wake. Mihogo ni bora zaidi kwa gharama zake nafuu daima, lakini ina kiasi kidogo sana cha madini ya chuma na zinki kinachohitajika kwa chakula cha afya. Aina za mihogo ya `VIRCA Plus` iliyoimarishwa lishe ina kiwango kikubwa cha madini haya kinachoweza kusaidia kupunguza `njaa ya siri` ya ukosefu wa utapiamlo.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu usalama

Unatumia teknolojia gani na kwa nini?Je, mihogo ya `VIRCA Plus` imekuzwa kwa Ugeuzi Jeni (GMO)?

Watafiti wa `VIRCA Plus` wanatumia teknolojia mbalimbali ili kuboresha mihogo, ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa kawaida wa mimea, uhandisi wa kimaumbile unaojulikana kama ubadilishaji au ugeuzaji jeni, (GMO) au bayotekinolojia, uchambuzi wa molekuli au uchunguzi wa jenomi (genomic).

Kwa mfano uzalishaji wa mimea kwa njia ya kawaida umetumiwa kwa ufanisi kuendeleza aina za mihogo ambayo inapingana na `CMD`. Lakini wazalishaji wa mimea wamekuwa na ufanisi duni wa ‘CBSD’, kwa hivyo wameendelea kutumia aina ambazo zinashikilia tu ugonjwa wa CBSD. Mihogo ya upinzani wa magonjwa bado inaweza kuonyesha dalili za virusi na kupata madhara kutokana na ugonjwa huo- na huweza kusababisha ugonjwa ukaenea zaidi.

Kwa hivyo, `VIRCA Plus` unatumia uhandisi wa kimaumbile kuingiza sehemu ndogo ya ugonjwa wa virusi wa milia ya kikahawia kwenye mihogo ili kuifanya mimea uweze kupingana dhidi ya ugonjwa huo kwa njia ya kuchanganya RNA (RNAi). RNAi imekuwa ikitumiwa kuendeleza idadi kadhaa ya mazao yenye upinzani wa ugonjwa, hasa kwa kuokoa kiwanda cha mapapai cha Hawaii kutokana na ugonjwa wenye madhara wa virusi wa `Ringspot. Wakati sifa bainishi zinazopingana na magonjwa ya virusi zinapochanganywa zote pamoja na aina zilizozalishwa za VIRCA Plus; wakulima wataweza kulima mihogo yenye upinzani dhidi ya magonjwa yote kwa mara ya kwanza.

Uhandisi wa ubadilishaji jeni pia ni zana muhimu kwa mihogo iliyoimarishwa lishe ya ‘VIRCA Plus’ kwa sababu haijaweza kuimarisha kiasi cha madini ya chuma na zinki kwenye mizizi ya mihogo kwa kutumia aina zilizopo za uzalishaji wa mimea kwa kufuata uzao (breeding lines). Katika ‘VIRCA Plus’, uhandisi wa kimaumbile unatumiwa kwa kuingiza jeni mbili kutoka kwenye mmea mwingine, ‘Arabadopsis’, ambao unatumika kuimarisha kiasi cha madini ya chuma na zinki kwenye mizizi ya mihogo. Uzalishaji pia utatumiwa kuingiza aina za sifa bainishi katika aina ya mazao ya kiwango cha juu yanayokidhi mahitaji ya wakulima na watumiaji.

Uchanganuzi wa molekuli na zana za kijenomi za uchunguzi hutumiwa katika miradi yote ili kuwajulisha watafiti kuhusu kuwepo ufanisi na usalama wa aina za ‘VIRCA Plus’ zikiendelezwa.

Je aina za mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itakuwa salama kwa wakulima kuipanda na kuitumia? Utajuaje?

Naam.

Kama mazao ya ubadilishaji wa kimaumbile; mihogo ya ‘VIRCA Plus’ inatathminiwa ili kujua usalama wa chakula na athari za kimazingira kulingana na taratibu za udhibiti wa kitaifa katika nchi shirika- Kenya, Nigeria na Uganda. Mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itapatikana kwa wakulima na watumiaji kwenye nchi tu ambayo shirika lake limeeleza kwamba mahitaji yote ya usalama wa taifa yametimizwa na ikaiidhinisha kutolewa.

Matokeo maalum kutoka kwenye majaribio ya shamba, uchambuzi wa maabara, na mafunzo mengine yanahitajika ili kuamua iwapo mazao ya bayotekinolojia ni salama kama mazao ya njia za desturi (kawaida).

Mara baada ya tafiti zote kukamilika, taarifa za ‘udhibiti’ zilizo na maelezo kuhusu usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’ utaandaliwa na kupelekwa kwa mashirika ya udhibiti katika kila nchi kwa ajili ya ukaguzi wao. Mihogo ya ‘VIRCA Plus’ inaweza kupatikana kwa wakulima na watumiaji katika nchi ikiwa tu shirika la udhibiti limehakikisha kwamba mahitaji yote ya usalama wa taifa yamezingatiwa ndipo huiidhinisha itolewe.

Je kusudi la majaribio shambani katika kupima usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’ ni nini?

Majaribio ya shambani yanafanywa nchini Kenya na Uganda ili kuzalisha data za udhibiti na kukusanya maelezo juu ya usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’. Kukiwa na marejeleo, idhini na usimamizi wa kawaida wa shirika la taifa la usalama, mihogo iliyojaribiwa shambani na mihogo ya kawaida ya aina moja inapandwa katika eneo hilo hilo ili taarifa za kilimo ziweze kukusanywa kwa aina zote (mbili) kwa kulinganisha.

  • Ikiwa mimea ya ‘VIRCA Plus’ na mimea ya kawaida itaonyesha tabia na ubora ulio sawa kwenye majaribio ya shamba, itadhihirisha kuwa mimea yote ni sawa isipokuwa mabadiliko yanayotarajiwa katika kupambana na magonjwa ya virusi vya mihogo.

Mara baada ya mafunzo yote kukamilika taarifa za ‘udhibiti’ zilizo na maelezo kuhusu usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itaandaliwa na kupelekwa kwa mashirika ya udhibiti katika kila nchi kwa ajili ya ukaguzi wao. Mihogo ya ‘VIRCA Plus’ inaweza kupatikana kwa wakulima na watumiaji katika nchi ikiwa tu Shirika la Udhibiti limehakikisha kwamba mahitaji yote ya usalama wa taifa yamezingatiwa ndipo huiidhinisha itolewe.

Je, uchunguzi wa maabara unasema nini kuhusu usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’?

Mizizi na majani ya mihogo ya ‘VIRCA Plus’ na mihogo ya desturi (kawaida) iliyopandwa kwenye majaribio ya shambani pia huchunguzwa katika maabara ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuthamini usalama. Viwango vya unyevu unyevu, wanga, protini, mafuta na virutubisho muhimu (hasa madini ya chuma na zinki na uimara wa lishe ya mihogo ya ‘VIRCA Plus’) utapimwa na matokeo yatalinganishwa. Viwango vya sumu asilia ya mimea (cyanogenic glycosides) pia vinatathminiwa: hizi ni sumu ambazo hutokea kwa njia za asili zinazopatikana katika mimea yote ya mihogo ambayo huondolewa katika mchakato sahihi wa kijadi wakati maandalizi ya chakula.

  • Kama tathmini zitaonyesha kwamba mimea ya ‘VIRCA Plus’ na mihogo ya kawaida ina kiasi sawa cha madini (kiwango cha juu cha chuma na zinki kwenye mihogo iliyoboreshwa lishe), inaonyesha kwamba aina zote ni salama na zina lishe bora inayolingana na ukila aina moja ni sawa na nyingine.

Chunguzi zingine zinazotumiwa kuonyesha kwamba mihogo ya ‘VIRCA Plus’ inaweza kukuzwa salama zinajumuisha upimaji tabia za kimolekuli, ambao ni uchambuzi wa DNA zinazoingizwa kwenye mihogo ya ‘VIRCA Plus’ na utulivu wake (uwezo wa kubakia bila kubadilika) kupitia vizazi vingine vya mmea.

Baada ya uchunguzi wote kukamilika, taarifa za ‘udhibiti’ zilizo na maelezo kuhusu usalama wa mihogo ya ‘VIRCA Plus’ itaandaliwa na kupelekwa kwa mashirika ya udhibiti katika kila nchi kwa ajili ya ukaguzi wao. Mihogo ya ‘VIRCA Plus’ inaweza kupatikana kwa wakulima na watumiaji wa nchi ikiwa tu shirika la Udhibiti limehakikisha kwamba mahitaji yote ya usalama wa taifa yamezingatiwa ndipo huiidhinisha itolewe.

Pakua Fact Sheet
Pakua FAQ’s