Na Dkt. Eliud Kireger
Kuboresha usalama wa chakula nchini kunahitaji mbinu kamili, pamoja na kuangalia vyakula vingine vikuu zaidi ya mahindi, mchele na ngano. Muhogo, zao kuu la tano ulimwenguni ni zao zuri mbadala. Licha ya umuhimu wake kama zao kuu katika usalama wa chakula, linaweza pia kutoa maelefu ya kazi kando ya msururu wa thamani kutokana na matumizi yake viwandani. Kwa hivyo mmea wa muhogo unaweza kutimiza juhudi za serikali ya Kenya kufikia malengo yake mawili ya maendeleo kati ya yale ‘Makubwa Manne’ – usalama wa chakula na utengenezaji bidhaa.
Kulingana na utafiti wa kina, mihogo itastawi wakati wa mabadiliko ya hewa, wakati ambapo vyakula vingine vikuu vingekabiliwa na changamoto. Wakulima katika pwani na magharibi mwa Kenya ambapo mihogo ni zao la pili muhimu zaidi la chakula baada ya mahindi, wanaweza kushuhudia haya. Zao hili hustawi vizuri wakati wa ukame wakati ambapo vyanzo vingine vichache sana vya chakula vinapatikana, kutoa usalama wa chakula na mapato ya ziada katika maeneo ya pembezoni yenye ukame mara kwa mara ambayo yanachukua karibu asilimia sabini na tano ya ardhi nchini Kenya. Kuhusiana na lishe, lishe ya mihogo hutoa mahitaji ya kiwango kamili cha nguvu inayohitajika kila siku na majani yake ni chanzo kikubwa cha protini. Mmea huu pia unaweza kuimarishwa ili kutoa virutubishi muhimu.
Licha ya umuhimu wa mihogo, mahindi bado hubakia kuwa sawa kwa utoshelevu wa chakula nchini Kenya. Kaya nyingi katika sehemu kadhaa za Kenya huzingatia kwamba mihogo ni zao la mtu maskini. Hata hivyo changamoto zinazoibuka katika uzalishaji wa mahindi kama ugonjwa wa virusi uitwao (necrosis) na ugonjwa wa viwavi huhitaji mabadiliko makubwa katika mazoea ya kula na kubadilisha mawazo. Tunahitaji kubadilisha msingi wa chakula chetu na kuwa makini kwenye mazao haya ya kitamaduni yenye uvumilivu zaidi kwa hali ya hewa.
Zaidi ya zao la kujikimu
Mihogo pia ni mmea unaoweza kuwa wa viwanda, hasa katika uzalishaji wa wanga, malisho ya wanyama, unga na ethanol (kemikali ya manukato na rangi). Uwezo huo wa muhogo haujachunguzwa vizuri hapa nchini Kenya. Kinyume chake, nchini Nigeria ambayo inaongoza ulimwenguni kwa uzalishaji wa mihogo, umezingatia kikamilifu kuiongezea mihogo thamani na faida kubwa za kiuchumi na kijamii. Matokeo yake, uzalishaji wa mihogo nchini humo ulifikia metriki za tani milioni 52 mnamo 2018. Kiwanda cha mihogo kimeajiri wakulima wananigeria zaidi ya milioni 6.
Nchini humo, viwanda vya biashara za kawaida vinapatikana katika baadhi ya maeneo kwa bidhaa zilizoongezewa thamani kama unga, keki, biskuti na vitu vingine vitamu vitamu. Mahitaji ya bidhaa hizi yanaongezeka kutokana na kubadilika kwa tabia za kula kwa jamii za mjini na za vijijini. Mihogo pia inaweza kutumiwa kuwa msingi wa wanga kwenye malisho ya wanyama, iliyo muhimu kwa kupunguza shinikizo la nafaka kama mahindi na ngano. Lakini usambazaji wa mazao uko chini daima. Maagizo ya hivi karibuni ya Wizara ya Kilimo ya kuchanganya mahindi na unga wa ngano na kiwango cha asilimia 10% ya mazao duni lakini yenye virutubishi kama mihogo, viazi, mtama na viazi vitamu ni hatua za mwelekeo sahihi wa matumaini kwenye uzalishaji.
Kulinda mavuno
Licha ya sifa zake bora, uzalishaji wa mihogo nchini Kenya na eneo la Afrika mashariki, unakabiliwa na changamoto mbalimbali, muhimu kati ya hizo ni kuwepo kwa magonjwa ya virusi na wadudu. Magonjwa makubwa ni pamoja na mosaiki (Mosaic) na kamba ya kikawia ambayo yanaweza kusababisha upoteaji wa mavuno hadi asilimia mia moja. Juhudi za msingi ni kukuza mimea ambayo inaweza kuvumilia magonjwa kama hayo. Wanasayansi wa Kenya kutoka katika Shirika la Utafiti la Kilimo na Mifugo la Kenya na Vyuo Vikuu vya Umma vinakuza aina sugu kwa kutumia teknolojia zote za kitamaduni na za kisasa kama vile Ugeuzaji Jeni (maumbile) (GM).
Majaribio ya shambani ya aina mpya sugu dhidi ya magonjwa chini ya shirika la Mihogo Sugu dhidi ya Virusi kwa ajili ya Afrika (VIRCA-Plus) yanafanyika katika maeneo mbalimbali nchini kote. Majaribio hayo, ambayo hufanywa chini ya idhini ya usimamizi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Uhai (NBA), huwawezesha watafiti kuchagua aina zilizoboreshwa zinazokidhi mahitaji ya wakulima, wakati huo wakiwahakikishia usalama wa mazingira na mihogo ya ugeuzaji jeni (GM) sheria inaagiza kupata ukubalifu wa mwisho kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Uhai (NBA) kabla ya mihogo hii mipya sugu kupitishwa na kulimwa shambani wazi wazi. Utafiti kama huo unafanyika pia nchini Uganda.
Mazao yetu makuu mayatima yanaleta uhai maishani tunashukuru juhudi za watafiti wa Kiafrika kwa kulinda mavuno yao kwa kupitia sayansi ya kukata makali. Walakini tunahitaji kuwaunga mkono watafiti wetu na kuweka mandhari ya sera zitakazowezesha jambo hili kufanyika.
Dkt. Eliud Kirenger ni Mkurugenzi Mkuu, Shirika la Utafiti wa Kilimo la Kenya.