Shirika la Utafiti la Kilimo na Mifugo Kenya (KALRO) limetuma maombi kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Usalama Uhai (NBA) ya kutolewa kwenye mazingira na kuweka kwenye masoko kwa mihogo  ambayo ni sugu dhidi ya Ugonjwa wa Kamba ya  Kikahawia wa mihogo. (CBSD)

 

Mihogo sugu dhidi ya Ugonjwa wa Kamba ya Kikahawia (CBSD) uliendelezwa chini ya ushirikiano wa kimataifa kati ya Shirika la Utafiti la Kilimo na Mifugo La Kenya (KALRO) na  Taasisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Rasilimali za Mazao ya Uganda (NaCRRI) na Kituo cha Sayansi cha Donald Danforth (DDPSC). Watafiti walitumia bayoteknolojia ya kisasa kwa kuingiza sehemu ndogo ya virusi viwili ambavyo vinasababisha Ugonjwa wa Kamba ya Kikahawia kwenye mmea wa mhogo ili kuufanya uwe sugu.

Mchakato ulitumia vifaa vinavyotumika kwa kuongeza utaratibu wa asili ya kinga dhidi ya virusi

Mihogo iliyoboreshwa ilitathminiwa zaidi ya kipindi cha miaka mitano, kwenye mashamba ya majaribio yaliyodhibitiwa (CFTs) katika sehemu  mbalimbali za Kenya na Uganda na vilionyesha kinga ya juu na uthabiti dhidi ya Ugonjwa wa Mihogo wa Kamba ya K.ikahawia kwenye mihogo (CBSD). Baada ya kuidhinishwa, mihogo hiyo itawekwa kwenye mipango ya kuzalisha mimea (mihogo) na aina zilizoboreshwa zitawafikia wakulima kwa kupitia mchakato wa kawaida wa serikali wa utoaji (mazao)

Wasaidie wakulima kupata aina za mihogo sugu dhidi ya ugonjwa wa Kamba ya Kikahawia ya Mihogo ( CBSD) kwa kujaza fomu  ya umma ya kushiriki  na kuituma kwa Mamlaka ya Usalama Uhai (NBA).Unaweza kuitoa fomu hapa.

Habari na Maoni

Machapisho Yetu

Video Zetu